Kiungo wa zamani wa Azam FC, Himid Mao Mkami amejiunga na klabu ya Tala'ea El Gaish SC ya Misri kwa mkataba wa miaka mitatu
Katika msimu uliopita, Mao aliitumikia Ghazl El Mahallah iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu Misri
Huu ni msimu wa tano Mao Mkami (30) anacheza ligi kuu ya Misri
Alikuwa mchezaji wa kutegemewa katika kikosi cha Ghazl El Mahallah akicheza mechi 27