Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wanatajwa kuwa mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Dikongue Mahop kutoka klabu ya Cannon Younde
Msimu wa 2022/23 Mahop aliibuka mfungaji bora wa Elite Ligi ya Cameroon akifunga mabao 15, assist 3
Mahop ana kasi, nguvu na maarifa ya kuwatoka mabeki. Anatumia vyema miguu yake yote miwili akiwa miongoni mwa washambuliaji wa timu ya Taifa ya Cameroon
Kabla ya kutua Cannone Younde, Mahop aliitumikia Fc Akonagui ambapo katika msimu wa 2019/20 alipachika mabao 24 na kutoa assist 5
Anatarajiwa kusajiliwa na Yanga kuchukua nafasi ya Fiston Mayele anayesubiri kujiunga na Pyramids Fc Misri



