Simba - Local

Simba yaweka hadharani mikakati SIMBA DAY

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Jul 2023
Simba yaweka hadharani mikakati SIMBA DAY

Klabu ya Simba imetangaza Wiki ya Simba itakayoanza Julai 29 ambayo kilele chake ni August 06 pale uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo kutakuwa na burudani zitakazohitimishwa na mchezo wa Kimataifa wa kirafiki

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed ametangaza kauli mbiu ya Simba Day ya mwaka huu ni UNYAMA MWINGI

Ahmed amesema Wiki ya Simba itazinduliwa rasmi Agosti Mosi eneo la Buza Kanisani wilayani Temeke ambapo atakuwepo na kispika chake ambacho amekuwa akitumia katika hamasa za kuwaita mashabiki uwanjani.

Katika wiki ya Simba kutakuwa na matukio mbalimbali ya kijamii kama kuchangia damu, kufanya usafi, kutembelea na kusaidia wagonjwa na watu wenye uhitaji

Lakini pia wiki ya Simba ya mwaka huu itatumika kuwakumbuka wakongwe waliowahi kucheza Simba zamani kwa kuwatembelea na kuzindua Matawi ya klabu

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia, Power Dynamo wamealikwa SIMBA DAY ambapo watacheza na Simba katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Aidha Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amesema siku ya Simba Day kibegi cha Simba kitapigwa mnada pamoja na jezi zake na mapato yatakwenda kusaidia kinamama Hospitali ya Muhimbili na Zanzibar

Benki ya CRDB itashirikiana na Simba katika kipindi chote cha wiki ya Simba pamoja na siku ya kilele August 06

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
26m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’