Droo ya hatua ya awali kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) imefanyika leo huko Misri
Azam FC itaanzia ugenini dhidi ya Bahir Dar Kenema ya Ethiopia hatua ya awali kisha kurudiana Dar es Salaam na mshindi atakutana na Club Africain ya Tunisia
Singida Fountain Gate FC itacheza mechi mbili za awali Kombe la Shirikisho Afrika(CAFCC) dhidi ya JKU ya Zanzibar na mshindi wa jumla atacheza dhidi ya Future FC ya Misri
Mechi za mkondo wa kwanza hatua ya awali zitapigwa mwishoni mwa August 2023



