Robertinho atamba Simba itampiga yeyote

Joel JJ By Joel JJ β€’ 26th July 2023


Robertinho atamba Simba itampiga yeyote

Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema msimu ujao wamejiandaa kukabiliana na timu yoyote watakayokutana nayo katika mashindano yote

Robertinho amesema Simba imeweka malengo makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano yote ikiwemo ligi ya mabingwa barani Afrika

Baada ya droo ya mechi za hatua ya awali na raundi ya kwanza kufanyika Misri jana, Simba inaanzia raundi ya kwanza ikiwa miongoni mwa timu nane kubwa barani Afrika ambazo hazitacheza mechi za awali

Robertinho amesema msimu huu wameweka malengo makubwa hivyo watakuwa tayari kucheza na Power Dynamos au African Sport katika raundi ya kwanza

"Simba iko tayari kushindani katika daraja la juu kabisa naweza kukwambia tuko tayari kushindana na hata Real Madrid. Tuna kila sababu ya kumuonyesha yeyote uwezo wetu ni kwa sababu sasa tuna wachezaji wazuri na benchi bora la ufundi"

"Tunawashimu wapinzani wetu lakini sisi tunafikiria mbali sana kwa sababu ukifikiria mbali basi nawe utafika mbali. Tunajiandaa kucheza katika hatua kubwa sana katika mashindano hayo," alisema Robertinho

Simba inaendelea na pre-season huko Uturuki ambapo kikosi kinatarajiwa kurejea nchini August 01 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea SIMBA DAY itakayofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa August 06


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.