Viongozi wa Bayern Munich wanasafiri kuelekea London kwa mazungumzo mapya na Tottenham kuhusu ofa ya £86m kumnunua mshambuliaji wa England Harry Kane, ambaye ametimiza umri wa miaka 30 leo siku ya Ijumaa. (Telegraph)
Paris St-Germain pia wako mguu sawa kumsajili Kane iwapo Tottenham wataamua kumuuza. (Sky Sports)
Manchester United wanaendelea na mazungumzo na Fiorentina kuhusu kiungo wa kati wa Morocco Sofyan Amrabat, 26, kuziba nafasi ya Mbrazil Fred, 30, anayetarajiwa kuondoka katika klabu hiyo. (90Min)
Chelsea imepata pigo katika mbio zake za kumsajili mshambuliaji wa Argentina mwenye umri wa miaka 29 Paulo Dybala ambaye anakaribia kusaini mkataba mpya na Roma. (Tuttomercatoweb)
Kiungo wa kati wa Italia Marco Verratti, 30, anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Al Hilal akitokea Paris St-Germain. (Fabrizio Romano)
Bayern wanavutiwa na kipa wa Brentford Mhispania David Raya, 27, na David de Gea, 32, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Manchester United. (Times)
Kiungo wa kati wa Ajax na Ghana Mohammed Kudus, 22, ameelezea mapenzi yake mkubwa ya kujiunga na Arsenal badala ya Chelsea. (Football transfers)
Chelsea imekataliwa ofa yake ya £24m kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Montpellier Mfaransa Elye Wahi, 20. (Standard)
The Blues wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Southampton raia wa Ubelgiji Romeo Lavia mwenye umri wa miaka 19 baada ya ofa yao ya pauni milioni 80 kwenda Brighton kwa ajili ya kiungo wa Ecuador Moises Caicedo kukataliwa. (Athletic)
Fulham wamewasilisha ombi la kumnunua winga wa Chelsea Muingereza Callum Hudson-Odoi, 22, kwa ada ya £4m. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa zamani wa Everton James Rodriguez anakaribia kujiunga na klabu yake ya 10. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anakaribia kuhamia Sao Paulo kama mchezaji huru. (Sun)
Kiungo wa kati wa zamani wa Aston Villa Arjan Raikhy, 20, anakaribia kusaini mkataba wa kujiunga na Leicester City. (Sky Sports)
BBC