Chelsea - International

Pochettino ajikita kuongeza vipaji Chelsea

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Jul 2023
Pochettino ajikita kuongeza vipaji Chelsea

Uhamisho wa wachezaji katika klabu ya Chelsea unakaribia kukamilika na klabu sasa inalenga kuleta vipaji vipya

Baada ya mkutano na mmiliki Todd Boehly, kocha Mauricio Pochettino na mkuu wa uajiri, walipitisha usajili wa kiungo Moises Caicedo wa Brighton

Brighton wanamthaminisha Caicedo kwa pauni 80m na Chelsea wako tayari kulipa kiasi hicho cha fedha. Caicedo amekubali masharti binafsi lakini mkataba bado haujasainiwa

Aidha Mshambuliaji wa kuchukua nafasi ya Christian Pulisic pia yuko kwenye ajenda na imeelezwa kwamba kufuatia ofa ya awali ya Β£20m, ambayo imekataliwa, mkutano mwingine na klabu ya Ufaransa Montpellier unapangwa kwa ajili ya Elye Wahi

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 atapelekwa kwa mkopo Strasbourg kwa miezi michache

Kiungo mshambuliaji wa Ajax, Mghana Mohamed Kudus pia yuko katika hesabu huku vyanzo mbalimbali vinathibitisha kuwa ofa ya kumnunua kiungo mshambuliaji na winga Michael Olise imetumwa kwa Crystal Palace

Wachezaji wawili wapya waliosajiliwa na Chelsea tayari wamemvutia Pochettino kwenye ziara ya majira ya kiangazi ya The Blues walipoilaza Brighton 4-3. Nicolas Jackson alifunga bao lake la kwanza na Christopher Nkunku pia amefunga mabao mawili katika michezo miwili

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
1h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
4h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
5h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
5h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
6h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
7h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
7h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
8h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’