Riyad Mahrez amekamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 30 kutoka Manchester City kwenda klabu ya Saudia Al Ahli - na sasa atalipwa pauni 750,000 kwa wiki kwa miaka miwili
City wamethibitisha kuwa dili hilo limetimia baada ya Al Ahli kufikia bei waliyoomba kwa winga huyo wa Algeria, ambaye alishinda mataji manne ya Ligi Kuu, mawili ya FA, matatu ya Carabao Cup na Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati alipokuwa Etihad baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa mara ya kwanza kwa Mkataba wa £60m kutoka kwa Leicester miaka mitano iliyopita
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 aliamua kutimkia Saudia baada ya Pep Guardiola kumuacha nje ya timu yake kwa fainali ya Kombe la FA na fainali ya Ligi ya Mabingwa huku The Blues wakishinda mara tatu msimu uliopita
Mahrez, ambaye pia alishinda Ligi ya Premia akiwa na Leicester, amesisitiza kwamba anaondoka bila majuto
"Kuichezea Manchester City imekuwa heshima na fursa. Nilikuja City kushinda mataji na kufurahia soka langu na nilifanikisha hayo yote na mengine mengi. Nimekuwa na miaka mitano isiyoweza kusahaulika na klabu hii ya soka, nikifanya kazi na wachezaji bora, mashabiki bora na meneja bora zaidi duniani"
"Nimejiwekea kumbukumbu nzuri maishani na namna tulivyoshinda taji la Ligi Kuu ya England na vita ambavyo tumekuwa navyo na Liverpool na, mwaka jana, Arsenal, ilisisitiza hamu na mawazo yetu ya kuwa bora zaidi. Manchester City daima itakuwa sehemu kubwa na yenye furaha maishani mwangu," alisema