Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Imani Kajula amesema kuwa aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Juma Mgunda, amebadilishiwa majukumu
Kajula amesema Mgunda sasa ni Mwalimu wa program maalum kwenye maeneo mbalimbali ya timu za vijana, wanawake na Senior kwa ajili ya kuisambaza falsafa ya Simba kwenye maeneo hayo
Kajula pia amesema Mgunda atakuwa Mkurugenzi wa maendeleo ya vijana chini ya miaka 17 na 20, timu ya wanawake na senior team
"Niwaambie wazi kuwa mwalimu Mgunda sasa hivi tunamtumia kwa program maalum, kwa hiyo mtamuona kwenye maeneo mengi sana"
"Tutamtumia kama mwalimu ambaye anazunguka kwenye timu zetu zote [U17, U20, Simba Queens na Simba senior team"
"Klabu yoyote kubwa huwa na mwalimu ambaye anafanya kazi zaidi ya moja kwa sababu lazima zile falsafa za timu zianzie kwenye timu za vijana hadi timu ya wakubwa lakini pia hata timu ya wanawake," alisema Kajula