Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Julai 30 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 30th July 2023


Tetesi za soka Ulaya, Jumapili Julai 30 2023

Liverpool wako kwenye mazungumzo na Paris St-Germain kuhusu kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kukataa uhamisho wa rekodi ya dunia wa £259m kwenda klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal.(Sunday Mirror)

Real Madrid wameweka kikomo kima cha euro 230m (£198m) kumnunua Mbappe kutoka Paris St-Germain kwa mkataba wa kudumu. (Marca - in Spanish)

Liverpool wanasalia kwenye mazungumzo na Southampton kuhusu kiungo wao wa kati wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19, baada ya kuona dau la awali la £34m pamoja na £4m la nyongeza limekataliwa. (Liverpool Echo)

Mwanamuziki nguli Jay-Z anajiandaa kununua Tottenham ikiwa mmiliki wa klabu hiyo Joe Lewis atapatikana na hatia kwa madai ya ulaghai na utoaji wa taarifa za ndani za kampuni kunakochukuliwa kuwa kinyume cha sheria. (Express)

Aston Villa wanapanga kumnunua winga wa Uhispania Adama Traore, 27 ambaye ni mchezaji huru kufuatia kuondoka kwake Wolves. (Football Insider)

Bayern Munich wanasalia na uhakika wa kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 30, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag amelazimika kufikiria upya mipango ya kumuuza mchezaji wa kimataifa wa Scotland Scott McTominay, 26, kwa West Ham kufuatia kuumia kwa kiungo mwenzake, Muingereza Kobbie Mainoo, 18, wakati wa ziara ya klabu hiyo nchini Marekani. (Telegraph)

Mkutano wa kilele unaohusisha mtendaji mkuu wa Bayern Jan-Christian Dreesen, mkurugenzi wa kiufundi Marco Neppe na mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy, utafanyika Jumatatu ambapo klabu hiyo ya Ujerumani itatoa ofa ya £75m kwa nahodha huyo wa Uingereza. (Mail)

Liverpool wanatazamiwa kukosa pauni milioni 7.5 za nyongeza zinazolipwa kutoka Bayern Munich iwapo mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 31, ataondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga na kujiunga na klabu ya Saudia ya Al-Nassr. (Mail)

Beki wa Uhispania Aymeric Laporte, 29, ataondoka Manchester City ikiwa watakamilisha usajili wa beki wa kati wa Croatia Josko Gvardiol, 21, kutoka RB Leipzig. (Manchester Evening News)

Paris St-Germain wamekataa matarajio ya kumuuza mlinzi wa Brazil Marquinhos, 29, huku klabu zikiwemo Al-Nassr zikivutiwa. (RMC - in French) Real Sociedad wameanza mazungumzo na Manchester United kumnunua kiungo wao wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 26. (AS - in Spanish)

Roma wamekubali dili la kumsaini mshambuliaji wa West Ham na Italia Gianluca Scamacca, 24, kwa mkopo na chaguo la pauni milioni 19 kumnunua. (Calciomercato - in Italian)

Aston Villa wanaendelea na juhudi zao za kumsajili Ferran Torres, 23 wa Barcelona, lakini kifurushi cha fedha kinachotolewa kwa mshambuliaji huyo wa Uhispania hakifikii matarajio yake. (Sport - in Spanish)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.