Simba yafunga pre-season kwa ushindi Uturuki

Joel JJ By Joel JJ β€’ 30th July 2023


Simba yafunga pre-season kwa ushindi Uturuki

Simba Sc imeunguruma huko Uturuki ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Batman AS katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki

Huo ulikuwa mchezo wa kuhitimisha pre-season ya takribani wiki tatu ambayo Simba waliweka huko Uturuki

Mabao ya Simba yalifungwa na Willy Onana, Saido Ntibazonkiza, Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' na John Bocco

Bocco na Kibu Denis wamekuwa na pre-season nzuri kila mmoja akipachika mabao mawili

Kibu alitoa pasi ya bao lililofungwa na Bocco wakati Ntibazonkiza, Fabrice Ngoma na Shomari Kapombe pia wakitia pasi za mabao mengine


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.