Ni rasmi aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele, amejiunga na klabu ya Pyramids Fc ya Misri
Pyramids wamemtambulisha Mayele kuwa mshambuliaji wao baada ya kukamilisha usajili wake kutoka Yanga
Ilikuwa misimu miwili bora kwa Mayele na klabu ya Yanga akifungwa jumla ya mabao 33 katika ligi kuu ya NBC
Mayele aliibuka mfungaji bora wa kombe la Shirikisho barani Afrika msimu uliopita akiweka kambani mabao saba
Pyramids wamemtambulisha na kumkabidhi jezi namba 9 ambayo alikuwa akitumia wakati yuko Yanga
