Tetesi za soka Ulaya, JUmatatu Julai 31 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
31 Jul 2023
Tetesi za soka Ulaya, JUmatatu Julai 31 2023

Arsenal wanaandaa mpango wa kumsajili mlinda lango wa Brentford Mhispania David Raya, 27. (Athletic) Bayern Munich pia wako tayari kuongeza juhudi zao za kumsajili Raya baada ya kukataa ofa ya mkopo. (Guardian)

Chelsea wanajaribu kufanya mazungumzo ya dili la fedha pamoja na mchezaji ili kumleta mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 24, Stamford Bridge msimu huu. (Record)

Mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 25, amesema alifikiria kuondoka katika klabu hiyo kabla ya meneja Erik ten Hag kuwasili msimu uliopita wa joto. (Athletic)

Winga wa Senegal Sadio Mane, 31, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Al-Nassr siku ya Jumatatu baada ya kukubaliana mkataba wa £24m kumsajili kutoka Bayern Munich. (Sky Sports)

Chelsea wana imani kwamba wanaweza kushinda katika kinyang'anyiro cha kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Michael Olise, 21, kutoka Crystal Palace. (90min)

Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez amekubali kusitisha mkataba wake na Gremio mwezi Desemba, huku Inter Miami wakitamani kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36. (Fabrizio Romano)

Mustakabali wa mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele huko Barcelona uko mashakani huku Paris St-Germain ikionesha nia ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Athletic)

Manchester City wana imani kwamba watakamilisha mpango wa kumnunua beki wa kati wa RB Leipzig na Croatia Josko Gvardiol, 21, kabla ya dirisha la kiangazi kufungwa. (Football Insider)

Crystal Palace wanakaribia kukamilisha dili la kiungo wa kati wa Flamengo na Brazil Matheus Franca, 19. (Fabrizio Romano) Beki wa pembeni wa Tottenham na Uhispania Sergio Reguilon, 26, ameonekana kulengwa na Real Sociedad. (Mail)

Arsenal wana nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ghana Mohammed Kudus mwenye umri wa miaka 22 kutoka Ajax. (Express)

Arsenal pia wameonesha nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Napoli na Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 22. (Football taransfers)

Nottingham Forest inafikiria kumnunua mlinda mlango wa Arsenal na Marekani Matt Turner, 29. (Athletic)

Wolves wanatayarisha ofa ya tatu na ya mwisho kwa kiungo wa kati Muingereza Alex Scott mwenye umri wa miaka 19 kutoka Bristol City baada ya ofa ya pauni milioni 18 na pauni milioni 20 kukataliwa. (Givemesport)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’