Bayern Munich iko tayari kuvunja rekodi ya euro milioni 80 (£68m) iliyoweka wakati ilipomnunua beki Mfaransa Lucas Hernandez, 27, ili kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 30, kutoka Tottenham. (Sky Sports)
Spurs huenda wakatumia hela itakayopatikana kutokana na mauzo ya Kane kuwanunua kiungo wa kati wa Barcelona na Ivory Coast Franck Kessie, 26, na mlinzi wa Ufaransa Clement Lenglet, 28. (Mundo Deportivo - kwa kihispania)
Tottenham pia wanamfuatilia mshambuliaji wa Nottingham Forest wa Wales Brennan Johnson, 22, mwenye thamani ya pauni milioni 50 ikiwa Kane atauzwa. (Mail)
Mmiliki mwenza wa Chelsea Todd Boehly anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Barcelona katika kutoa mkataba wa mchezaji pamoja na pesa taslimu kwa Paris St-Germain kwa mshambuliaji wao wa miaka 24 wa Ufaransa, Kylian Mbappe. (Independent)
The Blues pia wanatafuta mpango wa kubadilishana wachezaji unaomhusisha mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, na mshambuliaji wa Juventus Mserbia Dusan Vlahovic, 23. (Fabrizio Romano)
Liverpool wanatayarisha ofa iliyoboreshwa kwa kiungo wa kati wa Southampton na Ubelgiji Romeo Lavia mwenye thamani ya pauni milioni 50, huku Chelsea na Manchester United pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Mail)
Liverpool pia wanakaribia kukamilisha dili la kiungo wa Leicester City na Uingereza Trey Nyoni, 16. (Mirror)
West Ham wako tayari kuachana na mpango wa kumsajili kiungo wa Southampton mwenye thamani ya pauni milioni 40 James Ward-Prowse baada ya ombi la pili kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kukataliwa . (Guardian)
Burnley wako kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu mkataba wa mkopo wa msimu mzima kwa kiungo wa Ubelgiji Albert Sambi Lokonga, 23, wakati Auston Trusty, 24, pia anaweza kuondoka The Gunners, huku Sheffield United ikiongoza mbio za kumnunua beki huyo wa Marekani. (Telegraph - usajili unahitajika)
Paris-St Germain hawako tayari kukubali ofa ya thamani ya euro milioni 30 (£25.7m) kutoka kwa klabu ya Saudia Al-Hilal kwa ajili ya kiungo wao wa kati wa Italia Marco Verratti, 30. (Fabrizio Romano)
Al-Hilal pia wamewasilisha ombi la euro 140m (£120.3m) kumnunua mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24. (Sky Sports).
Chelsea wameanza mazungumzo rasmi na Brighton kuhusu usajili mlinda mlango wao wa Uhispania Robert Sanchez, 25. (Talksports)
Lakini Brighton bado hawajajibu ofa ya kwanza ya Chelsea kwa ajili ya Sanchez. (Atheletic- Usajili unahitajika) Chelsea wameweka bei ya pauni milioni 45 kwa beki Trevoh Chalobah, ambaye anakaribia kuhama klabu hiyo baada ya The Blues kuafikiana dili la kumsajili Mfaransa Axel Disasi, 25. Inter Milan wanavutiwa na Mwingereza huyo. (Evening Standard)
Everton wanamtaka mshambuliaji wa Southampton na Scotland Che Adams, huku Wolves na Bournemouth pia wakimfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Football Insider)
Nottingham Forest inamtaka mshambuliaji wa Rosario Central Muargentina Alejo Veliz, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Sky Italy - kwa Kiitaliano)
Barcelona wanaweza kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix, 23, ikiwa winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 26, atajiunga na Paris St-Germain. (Sport - kwa Kihispania)
BBC