Yanga - Local

Yanga yatamba, itashusha dozi kali

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Aug 2023
Yanga yatamba, itashusha dozi kali

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa wapinzani watakaokutana na Yanga msimu ujao wajipange kwelikweli kwani kuna timu zitashushiwa mvua ya mabao

Kamwe amesema kwa maandalizi ya kikosi aliyoyashuhudia Avic Town chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi, Wananchi wajiandae kwa msimu mwingine wa furaha Jangwani

"Kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi chini ya kocha Gamondi, mwishoni mwa wiki tulipata mchezo wa kirafiki dhidi ya Magereza Dar. Tunawaomba radhi Magereza Dsm kwa kipigo tulichowashushia ni mambo ambayo Gamondi anayaandaa kuelekea msimu ujao"

"Kwa maandalizi yanayoendelea na ari kubwa waliyonayo wachezaji, tunaamini msimu ujao goli zitakuja kama mvua. Tunaisubiri kwa hamu mechi ya nusu fainali Ngao ya Jamii, lengo letu ni kushinda ili twende fainali" alitamba Kamwe

Katika hatua nyingine, Kame amesema Yanga imemsajili mshambuliaji Hafiz Konkoni sio kwa lengo la kuvaa viatu vya Fiston Mayele

Kamwe amesema kama ilivyo kwa wachezaji wengine, Konkoni ametua Yanga ili asaidiane na wenzake ili kuhakikisha Yanga inafikia malengo yake na sio kuja kuvaa viatu vya Mayele

"Wakati tunamsajili Fiston Mayele hakuna mahala tulisema kuwa tumemsajili ili kuvaa viatu vya mchezaji fulani, ni hivyo hivyo kwa Hafiz Konkoni. Yeye amesajiliwa kwa kuzingatia mahitaji ya klabu na atashirikiana na wenzake ili kuhakikisha timu inashinda mechi zake"

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
4h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
4h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
8h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
12h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
13h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
14h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
15h ago
READ MORE β†’