Azam Fc kujipima na Bandari Fc

Joel JJ By Joel JJ β€’ 1st August 2023


Azam Fc kujipima na Bandari Fc

Baada ya kurejea kutoka Tunisia walikoweka kambi ya wiki tatu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya 2023/24, siku ya Jumamosi klabu ya Azam FC inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Bandari Fc kutoka nchini Kenya

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa 1 usiku

Utakuwa mchezo wa mwisho kwa Azam Fc kujipima kabla ya kuelekea mkoani Tanga kushiriki Ngao ya Jamii

August 09 Azam Fc itachuana na Yanga katika mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.