Singida Big Day inafanyika leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 2nd August 2023


Singida Big Day inafanyika leo

Singida Fountain Gate leo ipo kwenye tamasha lake la ‘Singida Big Day’ linaloendelea kwenye uwanja wa Liti, lakini kinachosubiriwa kwa hamu ni utambulisho wa nyota wake wapya akiwemo kiungo Mshambuliaji raia wa Togo, Marouf Tchakei (27) kutokea AS Vita

Singida imemnasa Tchakei kutoka Vita ikimpa mkataba wa miaka miwili na atatambulishwa leo sambamba na nyota wengine wapya wakiwemo, Joash Onyango, Gadiel Michael, Beno Kakolanya na Habib Kyombo kutoka Simba

Wengine wanaotarajiwa kutambulishwa leo ni Yahya Mbegu na Nicholas Wadada kutokea Ihefu, Dickson Ambundo aliyekuwa Yanga na Kelvin Kijiri kutokea KMC

Pia Walima Arizeti hao wa kanda ya Kati, watawatambulisha Mkenya Duke Abuya na Mnigeria Morice Chukwu sambamba na mastaa wengine

Pamoja na utambulisho huo, tamasha hilo linaloashiria kuwa tayari kwa kuanza msimu mpya ikiwa ni msimu wa pili kufanyika litahitimishwa na mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya wenyeji Singida Big Stars na AS Vita kutoka DR Congo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.