Arsenal imepata pigo baada ya mshambuliaji wake kiongozi Gabriel Jesus kuumia
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema Jesus atakosekana kwa wiki kadhaa akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu
"Alikuwa na shida katika goti lake ambalo lilimsababishia maumivu kwa hivyo ilibidi tumuache, atakuwa nje kwa wiki chache," alisema Arteta
Hii ni mara ya pili kwa Jesus kuumia kifundo cha mguu, ikumbukwe aliwahi kuumia Kombe la Dunia akiwa na Brazil na kumfanya kukosa baadhi ya mechi za Arsenal msimu uliopita