Yanga yacheza mechi mbili Avic Town

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th August 2023


Yanga yacheza mechi mbili Avic Town

Kikosi cha Yanga leo kimecheza mechi mbili za kirafiki katika uwanja wake wa mazoezi Avic Town

Asubuhi Yanga iliumana na Friends Rangers na kuibuka na ushindi wa mabao 6-1

Yanga imehitimisha mchezo wa pili jioni hii kwa kuumana na JKU ya Zanzibar mchezo uliomalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi aliomba mechi hizo kuwapima wachezaji wake wote

Yanga imehitimisha pre-season na sasa inasubiri kuelekea mkoani Tanga kuikabili Azam Fc katika mchezo wa Ngao ya Jamii


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.