Robertinho awaahidi furaha kwa mashabiki Simba

Joel JJ By Joel JJ β€’ 5th August 2023


Robertinho awaahidi furaha kwa mashabiki Simba

Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema Wanasimba watarajie burudani kutoka kwa timu yao katika Tamasha la Simba Day hapo kesho

Robertinho amesema anafahamu shauku ya mashabiki wa Simba ni kuiona timu yao. Amebainisha kuwa msimu huu watafurahi kwa sababu wana timu nzuri

"Nafahamu shauku ya mashabiki ni kuishuhudia timu yao. Nataka niwaambie tuna timu bora sana mwaka huu. Hii ni siku ya furaha kwa Wanasimba wote"

"Power Dynamos ni kipimo kizuri kwetu kwa kuwa ni mabingwa wa ligi ya Zambia na watashiriki michuano ya ligi ya mabingwa"

"Tuna mashindano mengi msimu huu, mchezo dhidi ya Power Dynamos utakuwa kipimo kizuri kwetu,"alisema

Nae beki Che Fondoh Malone amesema kwake ni heshima kubwa kushiriki Simba Day kwa mara ya kwanza

Malone amesema itakuwa siku kubwa na mashabiki watapata nafasi ya kuiona timu yao kwa mara ya kwanza pamoja na wachezaji wapya waliosajiliwa.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.