Klabu ya Saudi Arabia Al-Ittihad inapania kuwasilisha dau la euro milioni 60 kwa Liverpool ili kumpata Mohamed Salah na wako tayari kumlipa mshambuliaji huyo wa Misri mwenye umri wa miaka 31 euro milioni 180 kwa mkataba wa miaka miwili. (Al Riyadiah - kwa Kiarabu)
Ligi ya Saudia SPL inalenga wachezaji wakubwa zaidi ya Ligi ya Primia, mchezaji nyota wa Manchester City na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 32, kujiandaa kwa mashambulizi makubwa mwaka ujao. (Mirror)
Barcelona wamewasilisha ofa ya pamoja ya mkopo kwa Manchester City kuwasaka wachezaji wawili wa Ureno Joao Cancelo, 29, na Bernardo Silva, 28 - na wako tayari kuwanunua msimu ujao. (Sport - kwa Kihispania)
Juhudi za Arsenal kumpata mlinda mlango wa Brentford na Uhispania David Raya, 27, ziko katika "hatua ya mwisho" huku msaidizi wa The Gunners Mmarekani Matt Turner, 29, akitarajiwa kujiunga na Nottingham Forest. (Fabrizio Romano)
Lakini Nottingham Forest wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kipa wa zamani wa Leicester City Kasper Schmeichel, 36, kutoka Nice. (Eurosport Denmark)
Mshambulizi wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 24, ''yuko tayari'' kujiunga na Ligi ya Premia kwa mkopo wa msimu mmoja kabla ya kutimiza ndoto yake ya kuhamia Real Madrid. (Mirror)
Chelsea wako tayari kuwasilisha ofa iliyoboreshwa ya kumnunua kiungo wa Brighton Moises Caicedo baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ecuador mwenye umri wa miaka 21 kuachwa nje ya kikosi cha Seagulls kwa mechi yao ya kirafiki na Rayo Vallecano. (Telegraph - usajili unahitajika)
Beki wa Fulham Tosin Adarabioyo, 25, amepuuzilia mbali mpango wa kuhamia Tottenham huku beki huyo wa Uingereza akitaka kujiunga na Monaco ya Ufaransa badala yake. (Sun)
Klabu ya Uturuki Fenerbahce inavutiwa na kiungo wa Arsenal Jorginho, 31, huku kukiwa na tetesi kwamba Muitaliano huyo hajatulia kaskazini mwa London. (TRT - kwa Kituruki)
Bournemouth wamekataa ombi kutoka kwa wapinzani wao Ligi ya Primia West Ham kwa ajili ya mshambuliaji wao Muingereza Dominic Solanke, 25. (Daily Echo)
Burnley wameongeza ofa yao hadi pauni milioni 12 kwa kiungo wa Aston Villa Aaron Ramsey, 20, na pia wanamwinda beki wa Manchester United Muhispania Alvaro Fernandez, pia 20, kwa mkopo. (Mail)
Dau la West Ham la pauni milioni 25.9 kumnunua kiungo wa Ajax na Mexico Edson Alvarez, 25, bado halijafikia thamani ya klabu hiyo ya Uholanzi. (90 min)
Mpango wa Bournemouth wa pauni milioni 12 kumnunua kiungo wa kati wa Fiorentina Gaetano Castrovilli umezimwa baada ya Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 26 kushindwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. (Mail)
Nottingham Forest itaelekeza mawazo yao kwa mlinzi wa kati wa Corinthians, Murillo, 21, mwenye thamani ya pauni milioni 11, baada ya kushindwa kumsajili swahiba wake Roger Ibanez, 24, kutoka Roma. (Nottingham Post)
Leicester City wanaongeza juhudi zao za kumleta kwa mkopo mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea na Italia kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 katika kombe la dunia la Kiatu cha Dhahabu Cesare Casadei, 20. (Leicester Mercury)
BBC