Simba - Local

Simba DAY yaitikisa Dar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Aug 2023
Simba DAY yaitikisa Dar

Jana jiji la Dar es salaam lilisimama kwa saa kadhaa kupisha Tamasha kubwa la Michezo ukanda wa Afrika Mashariki na kati, SIMBA DAY

Ni rekodi juu ya rekodi kwa Simba, uwanja wa Benjamin Mkapa haukutosha kuwachukua watu wote waliojitokeza kushuhudia utambulisho wa kikosi cha Simba kwa ajili ya msimu wa 2023/24

Shamrashamra zikanogeshwa na ugeni wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ambaye aliwapongeza Simba kwa kuandaa Tamasha hilo kubwa

Tamasha hilo lilihitimishwa na mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Power Dynamos, mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia

Simba ikabuka na ushindi wa mabao 2-0, Willy Onana na Fabrice Ngoma wakifunga mabao hayo yaliyohitimisha kilele cha furaha ya mashabiki wa Simba baada ya kuona ubora wa timu yao

Onana ndiye alianza kuwapa furaha mashabiki wa Simba baada ya kufunga bao la kuongoza kipindi cha kwanza lililodumu hadi mapumziko huku bao la pili likifungwa kipindi cha pili

Kipindi cha kwanza Simba walianza kwa kasi wakipasiana pasi fupi fupi na kuonana walionekana wakitumia winga za pembeni kutengeneza mashambulizi

Mashambulizi yao yalikuwa yanasukwa na Willy Onana na Clatous Chama ambao walikuwa wanacheza kwa kubadilishana upande

Onana alionekana kuwavutia zaidi mashabiki wa Simba kutokana na namna alivyokuwa anapiga pasi za uhakika kwa kufikisha kwa mtu sahihi. Dakika ya 45 za kipindi cha kwanza zilithibitisha ufundi wake baada ya kukwamisha mpira nyavuni na kuwanyanyua mashabiki lukuki waliojitokeza kwa Mkapa

Mchezaji mwingine aliyewavutia Wanasimba ni beki wa kati Che Fondoh Malone aliyeonekana kuwa mahiri katika ulinzi pamoja na kuanzisha mashambulizi

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’