Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumanne August 08 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Aug 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne August 08 2023

Mshambuliaji wa Brazil Neymar ameiambia Paris St-Germain kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto na ndoto za mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ni kurejea Barcelona.(L'Equipe)

Chelsea wanaripotiwa kuwa katika mazungumzo wawakilishi wa Neymar kuhusu uwezekano wa kuhamia Stamford Bridge. (RMCSport)

Kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva anakaribia kuongeza mkataba wake kusalia Manchester City lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 yuko tayari kusubiri siku chache zaidi kuona Barcelona kama itapeleka ofa ya uhamisho. (Mundo Deportivo)

Liverpool italazimika kuilipa Southampton kiasi cha pauni milioni 50 kama wanataka kumpata kiungo wa kati Romeo Lavia mwenye umri wa miaka 19 kutoka St Mary's. (Sky Sports)

Liverpool hawajarejea tena nia yao ya kutaka kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Brazil wa Fluminense Andre, 22, wakati huu wakiendelea na mazungumzo na Southampton kuhusu mpango wa kumnunua Lavia. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 30, ataacha na mpango wa kuhamia Bayern Munich ikiwa vilabu hivyo viwili havitafikia makubaliano wiki hii. (Telegraph)

West Ham wamekubali mkataba wa pauni milioni 32 kumsaini kiungo wa kati wa Ajax na Mexico Edson Alvarez, 25. (Guardian)

Wakati huo huo, Manchester United wamekataa dau la pauni milioni 30 kutoka kwa The Hammers kwa ajili ya kiungo wa Scotland Scott McTominay, 26. (Manchester Evening News)

Mustakabali wa kocha wa West Ham David Moyes haujulikani huku kukiwa na hofu kwamba kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 anaweza kuondoka kama ataanza msimu vibaya au kama hatowaridhisha mashabiki wa timu hiyo. (Telegraph)

Beki wa England Harry Maguire, 30, anaweza kusalia Manchester United kwa msimu mwingine huku beki huyo wa kati akikataa kujiunga na klabu isiyoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya. (Football transfers)

United wanatumai kuwauza kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 26, na mchezaji wa kimataifa wa Brazil Fred, 30, wiki hii. (Mail)

Arsenal wamekataa ofa rasmi kutoka kwa Monaco kwa ajili ya mshambuliaji wa Marekani Folarin Balogun, 22. (Athletic)

Kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 31, anaweza kuondoka Arsenal na kujiunga na klabu ya Uturuki Fenerbahce licha ya kujiunga na The Gunners kutoka Chelsea kwa £12m mwezi Januari. (Times)

The Gunners pia wanaendelea na mazungumzo na Brentford kuhusu uhamisho wa mlinda mlango wa Hispania David Raya lakini Bayern Munich pia wanamtaka kipa huyo mwenye umri wa miaka 27. (Thats' Football via Twitter)

Chelsea wanajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Leeds United na Marekani Tyler Adams, 24, na wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21, kabla ya msimu huu kuanza. (Telegraph)

Chelsea na Juventus zimepanga duru mpya ya mazungumzo kujadili pendekezo la mkataba wa kubadilishana unaohusisha mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, na mshambuliaji wa Serbia, Dusan Vlahovic, 23. (Fabrizio Romano)

Wolves watafikiri kumteua kocha wa zamani wa Bournemouth Gary O'Neil, 40, kuwa meneja wao mpya ikiwa Mhispania Julen Lopetegui, 56, ataondoka katika klabu hiyo. (Sports)

Kiungo wa kati wa zamani wa Barcelona na Hispania Andres Iniesta, 39, anatazamiwa kutua katika Klabu ya Emirates inayoshiriki Ligi ya UAE hadi Juni 2024 kukiwa na nafasi ya kuongeza mwaka mwingine mmoja. (Fabrizio Romano)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’