Klabu ya Yanga jana ilizindua Documentary kwa ajili ya kumulika mafanikio waliyopata msimu uliopita katika mashindano mbalimbali
Katika msimu wa 20222/23, Yanga ilifanikiwa kushinda mataji yote ya ndani pamoja na kutinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Documentary hiyo inamulika kwa kina hatua kwa hatua yale yaliyokuwa yakijiri nyuma ya camera
Katika uzinduzi huo, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alisema wametengeza Documentary hiyo ili kuhifadhi katika kumbukumbu mafanikio ambayo walipata msimu uliopita hasa kucheza fainali ya kombe la Shirikisho la CAF
"Msimu uliopita tulipata mafanikio makubwa, kushinda mataji yote ya ndani na kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Yanga kufikia hatua hii naamini tulikuwa na kila sababu ya kuandaa Documentary hii ili kuhifadhi kumbukumbu hii kwa ajili ya vizazi vijavyo"
"Lakini pia Documentary hii imetoa nafasi kwa wengine kujifunza na kuona vile ambavyo tulipita milima na mabonde kuweza kufanikiwa kile tulichokipata"
"Sio nyakati zote zilikuwa za furaha, zipo nyakati ngumu ambazo tulipita, mashabiki wetu watapata kufahamu wakati mwingine ni kwa kiasi gani mambo sio rahisi kama yanavyoonekana nje," alisema Kamwe
Documentary hiyo itaonyeshwa na Azam Media kupitia Azam Max App kwa gharama ya Tsh 2,500/-



