Mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii, Yanga tayari wako jijini Tanga kwa ajili ya nusu fainali ya michuano hiyo dhidi ya Azam Fc
Mchezo huo utapigwa kesho Jumatano, August 09 katika uwanja wa Mkwakwani
Yanga iliwasili Tanga jana ikiwa na wachezaji wake wote wakiwa na mkakati wa kutetea Ngao hiyo ambayo wameishikilia kwa misimu miwili mfululizo
Wapinzani wao Azam Fc walikuwa walitangulia kutua mkoani Tanga mapema jana na timu hizo leo zitakamilisha maandalizi yao ya mwisho





