Ligi Kuu ya Uingereza yarejea leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 11th August 2023


Ligi Kuu ya Uingereza yarejea leo

Mikiki mikiki ya Ligi Kuu ya Uingereza imerejea ambapo mchezo mmoja unapigwa leo

Mabingwa watetezi Manchester City watakuwa ugenini kuikabili Burnley

Ni mchezo ambao utapigwa majira ya saa nne usiku kunako uwanja wa Turf Moor

Burnley kwa mara ya kwanza inaweza kuwatumia wachezaji waliosajiliwa majira ya kiangazi kama vile James Trafford, Zeki Amdouni, Sander Berge na Dara O'Shea

Michael Obafemi, ambaye amejiunga baada ya kucheza kwa mkopo Turf Moor msimu uliopita, hatakuwepo kutokana na tatizo la misuli ya paja

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasema beki wa kati wa Croatia Josko Gvardiol yuko tayari kucheza mechi yake ya kwanza baada ya kujiunga nao akitokea RB Leipzig kwa uhamisho wa £77m

Beki mwenzake Nathan Ake yuko fiti licha ya kukosa Ngao ya Jamii dhidi ya Arsenal kutokana na jeraha dogo. Kiungo Mateo Kovacic anaweza kucheza mechi yake ya kwanza ya ligi akiwa na City baada ya kuhama kutoka Chelsea mwezi Juni kwa kitita cha pauni milioni 25


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.