Simba - Local

Robertinho aipania Yanga, Ngao ya Jamii

Joel JJ By Joel JJ
12 Aug 2023
Robertinho aipania Yanga, Ngao ya Jamii

Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Mkwakwani

Robertinho amesema hakuna kitakachobadilika katika mbinu zake, watashambulia lango la wapinzani wao na kuhakikisha wanakuwa imara bila ya mpira

"Mimi sio kocha wa kuficha mbinu, malengo yangu ni kuona tunacheza zaidi katika lango la wapinzani na kuwa imara tunapokuwa hatuna mpira"

"Tunafahamu tunakwenda kucheza na timu tofauti na ile tuliyokutana nayo msimu uliopita, wana wachezaji wapya na benchi la ufundi, tumeweka mkakati mzuri wa kuhakikisha tunashinda"

"Nafurahi tuna kikosi imara, wachezaji wote wako tayari lakini tutawatumia wale ambao wako katika kiwango bora zaidi kwa wakati huu," alisema Robertinho

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, beki Israel Mwenda amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na wachezaji wote wako tayari kwa mchezo

"Maandalizi yamekamilika na wachezaji wote tuko tayari kwa mchezo, kila mmoja anafahamu umuhimu wa mchezo," alisema

Baada ya kuikosa Ngao ya Jamii kwa misimu miwili mfululizo mbele ya Yanga, msimu huu Simba imejipanga kushinda ngao hiyo katika uwanja wa Mkwakwani

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
23m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
2h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
12h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
13h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
20h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
21h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →