Klabu ya Simba imetangaza kumsajili golikipa Ayoub Lakred raia wa Morocco kuja kuungana na Ally Salim, Charles Abel na Aishi Manula katika nafasi ya mlinda mlango
Lakred mwenye umri wa miaka 28, anakuja kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Simba ambacho kina kibarua cha ligi ya ndani na ile ya kimataifa ikiwemo Africa Football League itakayoanza mwezi Oktoba
Mlinda lango huyo amewahi kuzitumikia AS FAR Rabat na RS berkane zote za Morocco




