Simba yatwaa Ngao ya Jamii

Joel JJ By Joel JJ β€’ 13th August 2023


Simba yatwaa Ngao ya Jamii

Simba imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa mikwaju 3-1 ya penati dhidi ya Yanga

Ulikuwa mchezo wa fainali ambao ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana baada ya dakika 90

Mlinda lango wa Simba Ally Salim alikuwa shujaa wa Simba akiokoa mikwaju mitatu ya penati katika mchezo ambao Simba haikuwa na dakika 90 bora

Baada ya kuikosa Ngao hiyo kwa misimu miwili, hatimaye mashabiki wa Simba leo wamefurahi kuishuhudia timu yao ikitwaa Ngao

Katika mchezo wa mapema kusaka mshindi wa tatu, Azam Fc iliichapa Singida FG mabao 2-0


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.