Mshambulizi wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 31, amekubali kandarasi ya misimu miwili na klabu ya Saudi Pro League ya Al-Hilal ambayo itampatia euro 160m (£138m) - mradi tu ada ya uhamisho itakubaliwa. (L'Equipe – in French)
Kiungo wa kati wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21, anaweza kufanyiwa vipimo vya afya katika klabu ya Chelsea Jumatatu kabla ya kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 115. (TalkSport)
Tottenham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Arsenal wa Marekani Folarin Balogun mwenye umri wa miaka 22 baada ya Harry Kane kuondoka. (Gazzetta Dello Sport – In Italian)
Liverpool, Bayern Munich na Paris St-Germain wanavutiwa na kiungo wa kati wa PSV Eindhoven mwenye umri wa miaka 25 aliyekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 32 Ibrahim Sangare. PSV ilikataa ofa kutoka Nottingham Forest msimu huu wa joto. (ESPN Uholanzi - kwa Kiholanzi)
Bayern Munich wamekataa ofa ya Manchester United ya kumnunua beki wa Ufaransa Benjamin Pavard, 27. (Sky Sports Deutschland – In Germany)
Manchester United wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Ubelgiji Amadou Onana, 21, na wanasubiri kujua bei yake kutoka kwa Everton. (Mail)
Ajax wanatazamiwa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa England wa wachezaji wa chini ya umri wa miaka 21 Chuba Akpom, 27, kutoka Middlesbrough kwa £10m. (Subscription - Athletic)
Beki wa Uingereza Kyle Walker, 33, atasaini mkataba mpya na Manchester City wiki hii na kukataa kuhamia Bayern Munich. (Fabrizio Romano)
Manchester City watamfikiria kiungo wa kati wa Crystal Palace na Mfaransa Michael Olise, 21, ikiwa watashindwa kumsajili kiungo wa kati wa West Ham na Brazil Lucas Paqueta, 25. (Football Insider)
Liverpool wanatarajiwa kufikia ofa ya Chelsea ya £55m kwa kiungo wa kati wa Southampton na Ubelgiji Romeo Lavia, 19. (TalkSport)
Juventus wako kwenye mazungumzo na Chelsea kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, ambaye ana nia ya kuhamia Turin. (Corriere Dello Sport - )
Mustakabali wa kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Eric Dier, 29, unaonekana kuwa shakani baada ya kuachwa nje ya kikosi cha meneja mpya Ange Postecoglou kwa sare ya 2-2 dhidi ya Brentford. (Mail)
Kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 26, anataka kusalia Barcelona maisha yote licha ya kuhusishwa na Manchester United. (El Periodico – in Spanish)
BBC