Pazia la Ligi Kuu ya NBC 2023/24 limefunguliwa leo ambapo mchezo wa mapema umeishuhudia geita Gold ikiandikisha ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuichapa Ihefu Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Ihefu huko Mbarali
Mshambuliaji Elias Maguli amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao msimu huu, akifunga bao pekee la ushindi kwa kichwa kwenye dakika ya tano ya mchezo
Namungo Fc itachuana na JKT Tanzania katika mchezo mwingine utakaopigwa leo huku Dodoma Jiji wakichuana na Coastal Union




