Afisa Habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema wamefanya maandalizi mazuri ya msimu mpya wakiwa tayari kufanya vizuri
Mtibwa Sugar itaanza msimu wa 2023/24 kwa kupambana na Simba SC, mechi itakayochezwa Agosti 17 katika uwanja wa Manungu
Kifaru amesema, wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya na wana imani ya watafanya vizuri
"Tupo tayari kwa mechi zote ambazo tutacheza, hatuhofii ndio maana tupo kwenye ligi, sio Young Africans, Simba SC au Azam FC"
"Tunatambua lazima tucheze na timu zote, Wapinzani wetu tunawaheshimu nasi tunafanya maandalizi kupata matokeo mazuri"
"Makosa ambayo yalifanyika msimu wa 2022/23 benchi la ufundi limeyafanyia kazi," alisema Kifaru



