Mchezo wa Ligi Kuu kati ya Azam Fc dhidi ya Kitayosce Fc umemalizwa dakika ya 19 baada ya wachezaji wa Kitayosce Fc kutokidhi taratibu za kinanuni kwa ajili ya mchezo huo kuendelea
Kitayosce waliingia uwanjani wakiwa na wachezaji nane na baadae wachezaji wao wawili wakaumia na hivyo kubaki sita uwanjani
Kanuni za FIFA haziruhusu mchezo kuendelea kama timu moja ina wachezaji pungufu ya saba uwanjani
Wakati mchezo huo unasitishwa Azam Fc walikuwa mbele kwa ushindi wa mabao 4-0, Feisal Salum akiwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu 'hat-trik' msimu huu
Bao la nne lilifungwa na Prince Dube



