Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kuhakikisha wananunua tiketi kutoka vituo rasmi na sio mikononi mwa watu
Kamwe ametoa tahadhari hiyo baada ya kuibuka kwa wauzaji wa tiketi feki
Kuelekea mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Asas Fc, Kamwe amesema ni vyema kuepuka kununua tiketi mikononi mwa watu
"Kumeibuka watu wanaouza tiketi feki, hivyo tunawatahadharisha mashabiki kuhakikisha wananua tiketi kutoka vituo halali"
"Jumapili ni siku ya kufungua msimu wetu wa ligi ya mabingwa. Matarajio yetu ni kuona mashabiki wakijitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao. Kwa uwezo wa uwanja wa Azam Complex, tunatarajia tutaujaza kabla ya siku ya mchezo yenyewe," alisema Kamwe
Akizungumza maandalizi ya kikosi, Kamwe amesema wachezaji wanaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo dhamira yao ikiwa ni kuibuka na ushindi mnono