Chelsea wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Marekani Folarin Balogun kutoka Arsenal, ambaye thamani yake ni £50m, huku Monaco pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, huku Inter Milan wakijitoa kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka. ( Sky Sports)
Chelsea wanataka kumnunua beki wa kulia wa Real Valladolid na Uhispania Ivan Fresneda lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 anataka kuhamia Barcelona. (Mail)
Manchester City wana imani winga wa Ureno Bernardo Silva, 29, atasaini mkataba mpya licha ya uvumi kuhusu mustakabali wake msimu huu. (90 min)
The Blues pia wanakaribia kutoa kitita cha pauni milioni 11.8 kwa mlinda mlango wa Serbia na New England Revolution Djordje Petrovic, 23. (Evening Standard)
Fiorentina bado hawajapokea ofa rasmi kutoka kwa Manchester United kwa kiungo wa kati wa Morocco Sofyan Amrabat, 26. (Mirror)
Barcelona wapo kwenye mazungumzo ya kiwango cha juu na Manchester City ili kumsajili beki wa Ureno Joao Cancelo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anataka kuhama. ( Fabrizio Romano)
Luton wametuma ya maombi ya kutaka kujua kuhusu mkopo kwa mlinzi wa Tottenham Hotspur Muingereza Japhet Tanganga, 24 (Athletic - subscription required)
Mlinzi wa Manchester United na Ufaransa Raphael Varane, 30, anasakwa na klabu ya Saudi Arabia Al-Ittihad. ( Express)
Mshambulizi wa Barcelona Mhispania Ansu Fati, 20, amepewa ofa ya kwenda Paris St-Germain baada ya hapo awali kuhusishwa na Manchester United na Arsenal. (Sun)
Benjamin Pavard wa Bayern Munich , 27, anasalia kuwa mmoja wapo wa wachezaji wanaolengwa na Inter Milan huku beki huyo wa Ufaransa akiivutia pia Arsenal . (Evening Standard)
Mkufunzi wa West Ham David Moyes amedai kuwa kwa sasa hafikirii kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 30 na nyota wa zamani wa Hammers Jesse Lingard. (Mail)
Southampton wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Luca Kerber mwenye umri wa miaka 21 kutoka Saarbrucken. (Mail)
BBC