Kuna makubaliano kimsingi kwa mlinzi wa kulia wa Ureno Joao Cancelo, 29, kujiunga na Barcelona kutoka Manchester City kwa mkopo wa awali wa msimu mzima. (SPORT)
Chelsea imefanya mawasiliano na washauri wa mshambuliaji wa Marekani aliyekadiriwa kuwa na thamani ya £50m, Folarin Balogun, 22. (TalkSport)
Mlinzi wa kushoto wa Arsenal Nuno Tavares, 23, anatafuta chaguzi nyingine baada ya pendekezo la kuhamia Nottingham Forest kuwa gumu. (Fabrizio Romano)
The Gunners hawana nia ya kumuuza kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey, 30, huku kukiwa na nia ya pande za Saudi Pro League pamoja na Juventus na Fenerbahce. (Express)
Paris St-Germain wamekubali masharti binafsi kwa mkataba wa miaka mitano na mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Randal Kolo Muani, 24. (Foot Mercato)
West Ham United imekuwa na ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Ghana Mohammed Kudus, 23, iliyokataliwa na Ajax. (The Athletic)
Hata hivyo, West Ham wamekubali ada ya takribani £19m ikijumuisha nyongeza na Stuttgart kwa ajili ya mlinzi wa Ugiriki Konstantinos Mavropanos, 25. (Sky Sports)
Mlinda lango wa Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 31, anakaribia kusaini mkataba mpya na Barcelona ambao utamweka katika klabu hiyo hadi 2028. (ESPN)
Celtic sasa wako katika nafasi nzuri zaidi ya kumnunua tena mlinzi wa kushoto wa Arsenal Kieran Tierney, 26, baada ya Newcastle United kumaliza nia yao ya kumnunua mlinzi huyo wa Scotland. (Football Insider)
Aaron Wan-Bissaka, 25, hataondoka Manchester United msimu huu wa joto kwani anataka kupigania nafasi ya beki wa kulia chaguo la kwanza huko Old Trafford. (Mail)
Lakini kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 26, na mlinzi wa kushoto wa Uingereza Brandon Williams, 22, wote wanaweza kuondoka Manchester United na kwa sasa hawafikiriwi kuchaguliwa. (Manchester Evening news)
Inter Milan wanashinikiza kumsajili beki wa kulia wa Ufaransa Benjamin Pavard kutoka Bayern Munich - lakini Thomas Tuchel anataka kumbakisha beki huyo mwenye umri wa miaka 27 nchini Ujerumani. (Sky Sports)
Leeds United inapanga kumuuza mlinda lango wa Ufaransa Illan Meslier, 23, kabla ya mwisho wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Football Insider)
Mlinzi Eric Bailly pia anaweza kuondoka, huku Manchester United wakiwa kwenye mazungumzo na Fulham kuhusu mpango wa kumnunua beki huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 29. (Mail)
Klabu ya Saudi Pro League, Al-Ahli inashinikiza kumsajili kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Italia Marco Verratti, huku makubaliano kati ya mchezaji na klabu yakiwa tayari. (L'Equipe) Sunderland wana nia ya kumsajili mshambuliaji chipukizi wa Uingereza Jay Stansfield mwenye umri wa miaka 20 kutoka Fulham. (Chronicle Live)
Inter Milan wanashinikiza kumsajili beki wa kulia wa Ufaransa Benjamin Pavard kutoka Bayern Munich - lakini Thomas Tuchel anataka kumbakisha beki huyo mwenye umri wa miaka 27 nchini Ujerumani. (Sky Sports)
BBC



