Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu August 21 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st August 2023


Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu August 21 2023

Manchester United wanafikiria kumnunua kiungo wa Paris St-Germain na Italia Marco Verratti, 30, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Al-Ahli ya Saudia na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich. (L'Equipe, via Mirror)

United pia inachunguza dili la mlinda mlango wa Ugiriki Odysseas Vlachodimos huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akitarajiwa kuondoka Benfica. (Fabrizio Romano)

Rennes wamekataa ombi la kwanza kutoka kwa West Ham kumnunua winga wa Ubelgiji Jeremy Doku, 21, ambaye pia amevutia Manchester City. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)

Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Olmo, 25, anasema "anaridhika" kuwa RB Leipzig baada ya kuhusishwa na uhamisho wa Manchester City kama mbadala wa Kevin de Bruyne aliyejeruhiwa. (Bild - kwa Kijerumani)

Aston Villa wanatathmini dau la kumnunua beki wa kushoto wa Arsenal na Ureno Nuno Tavares, 23, kama mbadala wa mlinzi wa Sevilla mwenye umri wa miaka 31 na Argentina Marcos Acuna. (Fabrizio Romano)

Sevilla wanataka kumsajili kiungo wa kati wa West Ham Mhispania Pablo Fornals, 27, ambaye yuko katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake na itagharimu kati ya £4.3m na £6.8m. (AS - kwa Kihispania)

Nottingham Forest iko tayari kulipa £15m kwa mshambuliaji wa Botafogo Matheus Nascimento, lakini Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 19 anataka uhamisho wake ufanyike Januari ili kusaidia timu yake kushinda taji la Serie A la Brazil. (Sun)

Everton wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Southampton Che Adams, 27 kutoka Scotland . (Telegraph - usajili unahitajika)

Beki wa pembeni wa Marekani Sergino Dest, 22, atahama kwa mkopo kutoka Barcelona kwenda PSV Eindhoven baada ya mabingwa hao wa La Liga kukubali kulipa 50% ya mshahara wake. (Fabrizio Romano)

Barcelona wanamfuatilia winga wa Bayern Munich wa Ujerumani Leroy Sane na wanaweza kutuma ofa ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 msimu ujao. (Bild, via Goal)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.