Mshambuliaji wa Simba Moses Phiri ameeleza furaha yake baada ya kufunga bao lake la kwanza msimu huu
Phiri aliweka kambani bao la pili jana katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji akimaliza ukame wa kutofunga kwa muda mrefu
Phiri ambaye alikosa robo tatu ya duru ya pili msimu uliopita kutokana na majeraha, amesema bado yupo sana Simba
"Nimefurahi sana kufunga bao langu la kwanza msimu huu. Baada ya kutokana kwenye majeraha nimekaa muda mrefu pasipo kufunga lakini bao nililofunga jana limeniongezea ari. Naamini tutakuwa na msimu bora sana"
"Nawashukuru mashabiki wa Simba kwa sapoti yao kwangu, wasiwe na wasiwasi kwa sababu bado nipo sana. Nina mkataba na Simba, naheshimu mkataba wangu. Pamoja na kwamba sipati nafasi ya kucheza mara kwa mara, nafahamu ni jukumu la kocha ninachopaswa kufanya ni kuendelea kupambana na kuisaidia timu yangu pale ninapopatiwa nafasi," alisema Phiri
Phiri alimaliza msimu uliopita akiwa kinara wa kuzifumania nyavu katika mashindano yote kwenye kikosi cha Simba
Msimu huu amekuwa na nafasi finyu kwenye kikosi cha kwanza lakini tayari ana bao moja kwenye akaunti yake ya magoli



