Yanga - Local

Gamondi alia na safu ya ushambuliaji Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Aug 2023
Gamondi alia na safu ya ushambuliaji Yanga

Licha ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Asas Fc katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema hakuridhishwa na idadi ya mabao ambayo walifunga katika mchezo huo

Stephane Aziz Ki na Kennedy Musonda walifunga mabao ya Yanga katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi Yanga ikitawala wakati wote

Gamondi amesema kipindi cha kwanza vijana wake hawakucheza katika ubora wao lakini kipindi cha pili walirejea wakiwa bora zaidi na pengine walistahili kufunga mabao zaidi ya matano

"Nimefurahi tumeshinda lakini sikuridhishwa na umakini katika matumizi ya nafasi. Kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri sana lakini kipindi cha pili tulitawala mchezo kutengeneza nafasi nyingi. Pengine tulipaswa kufunga mabao matano hata sita"

"Wapinzani wetu hawakutaka kucheza mpira kwenye kipindi cha pili, zaidi walijiangusha na kutumia kila mbinu kutupunguza kasi, jambo muhimu tumeshinda"

"Tuna dakika nyingine 90 mwishoni mwa wiki nafikiri tunaweza kumaliza mchezo huu na kusonga mbele hatua inayofuata," alisema Gamondi

Gamondi amesema wataendelea kufanya maboresho katika safu ya ushambuliaji ili kuhakikisha wanatumia vyema nafasi wanazotengeneza

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’