Simba kumpa mkono wa kwaheri Banda

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd August 2023


Simba kumpa mkono wa kwaheri Banda

Mashabiki wa Simba wasitarajie kumshuhudia winga Peter Banda akiendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Ngao ya Jamii

Simba inatarajiwa kumruhusu mchezaji huyo kwenda kusaka changamoto sehemu nyingine

Ni baada ya kukamilisha usajili wa mlinda lango Ayoub Lakred kutoka klabu ya FAR Rabbat ya Morocco

Simba inapaswa kuengua jina la mchezaji mmoja ili kusalia na wachezaji 12 ili kukidhi kanuni za shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Dirisha la usajili la ndani pamoja na lile la CAF yote yatafungwa August 31

Banda huenda akatimkia Ufaransa kuungana na Pape Ousmane Sakho ambaye Simba ilimuuza klabu ya Union Sportive Quevillaise-Rouen Metropol inayoshiriki ligi daraja la kwanza


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.