Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatano August 23 2023

Joel JJ By Joel JJ
23 Aug 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatano August 23 2023

West Ham bado wana matumaini ya kumsajili mchezaji wa Ajax, Mohammed Kudus baada ya ombi lao la awali la kiungo huyo wa kati wa miaka 23 kukataliwa. (Sky Sports)

The Hammers wamewasilisha ofa ya pili ya £35.8m (euro 42m) ya kumnunua Kudus lakini imekataliwa na Ajax. (Fabrizio Romano)

Ofa ya Liverpool ya pauni milioni 25.6 (euro 30m) kwa ajili ya kiungo wa Brazil Andre, 22, imekataliwa na Fluminense ambao wanasitasita kumpoteza mchezaji huyo kabla ya kumalizika kwa msimu wao wa ligi mwezi Desemba. (ESPN)

Manchester City huenda wakafufua mkataba wa pauni milioni 80 na West Ham kwa kiungo wa kati wa Brazil Lucas Paqueta, 25, mwezi Januari, mara tu uchunguzi wa Chama cha Soka kuhusu madai ya ukiukaji wa sheria ya kamari ya mchezaji huyo kukamilika. (Sky Sports)

Fiorentina wamempa kiungo wa Morocco Sofyan Amrabat, 27, hadi Ijumaa kuamua kama anataka kusalia katika klabu hiyo huku Liverpool huku Manchester United na Atletico Madrid zikimuwania. (Corriere dello Sport via Football Italia)

Mustakabali wa kiungo wa kati wa Buyern Munich Mholanzi Ryan Gravenberch anayewaniwa na Liverpool uko mashakani huku klabu hiyo ya Bundesliga ikikaribia kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (The Athletic - Usajili unahitajika)

Arsenal wamewafahamisha wawaniaji wa Saudi Arabia na Real Madrid kwamba mlinzi wao Mbrazil Gabriel, 25, hapatikani. (Mirror)

Bernardo Silva, 29, ametia saini mkataba mpya katika klabu ya Manchester City, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno akijitoa kwa mabingwa hao wa Ligi ya Primia hadi Juni 2026. (Fabrizio Romano).

Meneja mkuu wa Roma Lina Souloukou amesafiri kwa ndege hadi London, na hivyo kuchochea uvumi wa mazungumzo na Chelsea kuhusu mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30. (Tuttomercatoweb - kwa Kiitaliano)

Lukaku kwa sasa anafanya mazoezi na wachezaji wa chini ya miaka 21 wa Chelsea na hata hajazungumza na kocha mpya Mauricio Pochettino, huku klabu hiyo ikikataa kumruhusu kuondoka tena kwa mkopo. (Telegraph - usajili unahitajika)

Everton wamejiondoa katika mpango wa kumnunua winga wa Chelsea na Muingereza Callum Hudson-Odoi, 22, lakini The Toffees wanasalia kwenye mazungumzo na Southampton kuhusu mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Scotland Che Adams, 27. (Liverpool Echo)

Manchester United wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Fenerbahce na Uturuki Altay Bayindir, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akiwa na kipengele cha kumuachia cha £4.2m. (Mail)

Bayindir amefanyiwa uchunguzi wa awali wa matibabu nchini Ugiriki kuhusu tatizo la mgongo lililopo, ambalo matokeo yake yataamua iwapo United itaendeleza mpango huo. (Star)

Klabu kadhaa za Ligi ya Premia zinafuatilia hali ya mshambuliaji wa Uhispania Ansu Fati katika klabu ya Barcelona huku klabu hiyo ikijiandaa kwa mazungumzo na wakala Jorge Mendes kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Sport - kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa Leicester City Mnigeria Kelechi Iheanacho, 26, ameibuka kama mlengwa mkuu wa klabu ya Crystal Palace. (Leicestershire Live)

Manchester United na Chelsea zimeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Croatia Dino Klapija mwenye umri wa miaka 16 kutoka Kustojia. (Mail)

BBC

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
24m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
2h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
12h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
13h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
20h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
21h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →