Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mchezo mmoja utapigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watakuwa wenyeji wa KMC katika mchezo wa derby
Utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga msimu huu 2023/24 wakati KMC watakuwa wakicheza mechi yao ya pili msimu huu
Walianzia Ruangwa ambako walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo Fc
Ni mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali, wenyeji Yanga wakipewa nafasi zaidi kutokana na ubora wa kikosi chao
Yanga imetoka kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Asas Fc katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika
Wakiwa mabingwa watetezi watataka kuanza vyema msimu ili kuwasogelea watani za Simba walio kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kushinda mechi zao zote mbili za kwanza
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi kwa mara ya kwanza ataiongoza timu hiyo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambayo pia inaongozwa na Kocha mpya Abdihamid Moalin ambaye amewahi kuinoa klabu ya Azam Fc



