Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi August 26 2023

Joel JJ By Joel JJ
24 Aug 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi August 26 2023

Manchester City inatathmini mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Matheus Nunes, 24, kutoka Wolves. (Athletic)

Kuna uwezekano mkubwa wa Wolves kumruhusu Nunes kuondoka Molineux endapo Manchester City watatoa ofa kubwa kwa mchezaji huyo. (Express & Star)

City pia wameelekeza darubini yao kwa kiungo mshambuliaji wa Crystal Palace na England Eberechi Eze, 25, baada ya kusitisha mpango wao wa kumnunua kiungo wa West Ham wa Brazil Lucas Paqueta, 25. (Times - usajili unahitajika)

Fluminense haitamuuza kiungo Mbrazil Andre mwenye umri wa miaka 22 mwaka wa 2023 licha ya Liverpool, Fulham na Sporting Lisbon kumtaka . (O Globo - kwa Kireno)

Mshambuliaji wa Arsenal na Ivory Coast Nicolas Pepe, 28, anatarajiwa kuhamia Saudi Arabia baada ya kukataa nafasi ya kujiunga na Besiktas. (RMC kupitia Metro)

Chelsea itamsihi mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, kukubali ofa kutoka Saudi Arabia iwapo makubaliano hayawezi kufikiwa na klabu mojawapo ya Ulaya. (Talksport)

Juventus wako tayari kulipa Chelsea £35m kwa ajili ya Lukaku lakini Waitaliano hao wanatarajia kupata £50m kutokana na mauzo ya mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 23, kabla ya kuendelea na mpango huo. (Standard)

Lazio wamesitisha azma yao ya kumsajili mlinda mlango wa Tottenham mwenye umri wa miaka 36 Hugo Lloris. (Fabrizio Romano)

West Ham bado wako kwenye mazungumzo na Ajax kuhusu mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Ghana Mohammed Kudus mwenye umri wa miaka 23 baada ya ofa mbili kukataliwa. (Telegraph - usajili unahitajika)

West Ham pia wameanzisha mazungumzo na Sevilla kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Morocco Youssef En-Nesyri, 26. (Sky Sports)

Brentford wamewasilisha ofa ililoboreshwa ya kumnunua winga wa Fiorentina Nico Gonzalez lakini klabu hiyo ya Serie na hata Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 21 hana haja ya kufanya mazungumzo ya uhamisho. (Football Italia)

Sheffield United wanakaribia kumnunua mshambuliaji wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 21 Cameron Archer kwa pauni milioni 18.5. (Guardian)

Tottenham wamepinga jaribio ya Barcelona kumsajili kwa mkopo kiungo mshambuliaji wa Argentina Giovani Lo Celso, 27. (Sport - kwa Kihispania)

Wakala mkuu Jorge Mendes anatarajiwa Barcelona ili kukamilisha uhamisho wa beki wa pembeni wa Ureno Joao Cancelo kutoka Manchester City hadi Nou Camp. (AS - kwa Kihispania)

Burnley na Granada zimeonesha nia ya kutaka kumsajili beki wa Manchester United Mhispania mwenye umri wa miaka 20 Alvaro Fernandez. (Mirror)

Everton bado inajadiliana na Southampton kuhusu uhamisho wa mchezaji wa Scotland Che Adams, 27, lakini hawatamnunua mshambuliaji wa Troyes, 27, kutoka Guinea-Bissau, Mama Balde. (Liverpool Echo)

BBC

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
9h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
10h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
12h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
12h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
13h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
13h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
14h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
14h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
14h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
16h ago
READ MORE →