Aliyekuwa beki wa Yanga, Abdalla Haji Shaibu 'Ninja' amejiunga na FC Lubumbashi ya DR Congo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo
Shaibu ametua Lubumbashi akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika. Ninja amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili
Shaibu ameungana na wachezaji kama George Mpole (Fc Lupopo) na Said Khamis (AS Vita) Watanzania ambao wanashiriki ligi kuu ya DR Congo
Mbali na kuitumikia Yanga kwa vipindi viwili tofauti, Shaibu pia amewahi kuitumikia LA Galaxy inayoshiriki ligi kuu ya Marekani akicheza na nyota kama Zlatan Ibrahimovic
Awamu yake ya pili na Yanga hakuwa na wakati mzuri wa kucheza kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimsumbua mara kwa mara