Pluijm ajiengua Singida FG

Joel JJ By Joel JJ • 30th August 2023


Pluijm ajiengua Singida FG

Jana klabu ya Singida FG ilitangaza kuondoka kwa Kocha wake mkuu Hans van Pluijm ikiwa ni siku chache baada ya kupoteza mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya JKU kwa kufungwa mabao 2-0 

Hata hivyo Singida FG ilisonga mbele raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Singida FG, zimebainisha kuwa Pluijm alijiuzulu mwenyewe baada ya kipigo hicho

Kocha huyo raia wa Uholanzi ameiongoza Singida FG tangu msimu uliopita, akiisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya nne kwenye ligi kuu ya NBC msimu uliopita

Taarifa ya Singida FG imebainisha kuwa kocha Mathias Lule atakuwa Kaimu Kocha Mkuu wakati uongozi ukiendelea kusaka kocha mpya


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.