Simba - Local

Simba kushirikiana na ubalozi wa Uturuki

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Aug 2023
Simba kushirikiana na ubalozi wa Uturuki

Jana viongozi wa klabu ya Simba walimtembelea Balozi wa Uturuki nchini, Dkt. Mehmet Gulluoglu kwa ajili ya kutoa shukrani kwa ushirikiano ambao ubalozi huo ulitoa wakati Simba ilipoweka kambi ya maandalizi ya msimu nchini Uturuki

Simba imedhamiria kujenga uhusiano endelevu baina yake na Serikali ya Uturuki kupitia Ubalozi wa nchi hiyo

Katika mazungumzo hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Salim Abdallah alimshukuru Balozi wa kwa ushirikiano mkubwa walioonyesha na kuahidi kuendeleza ushirikiano mbalimbali na klabu ya Simba ikiwemo soka la vijana, timu ya wakubwa na timu ya wanawake

Kwa upande wake balozi wa Uturuki, Dr. Mehmet Gulluoglu alishukuru Klabu ya Simba kwa kuchagua Uturuki kama sehemu ya kuweka kambi yake kabla msimu kuanza na ameahidi kushirikiana na Simba katika maeneo mbalimbali

Kwenye ziara hiyo ya ubalozi wa Uturuki pia alikuwepo Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangugu, Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula, Mkuu wa Oparesheni za Mpira, Mathew Shayo na Mkuu wa Utawala wa Klabu ya Simba, Belinda Paul

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
2h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
6h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
7h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
8h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
8h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
9h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
9h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’