Aliyekuwa winga wa Simba Peter Banda amerejea katika klabu yake ya zamani, Nyasa Big Bullets ya Malawi
Mapema wiki hii Simba ilitangaza kuachana na Banda baada ya makubaliano ya pande mbili
Awali kulikuwa na taarifa kuwa angetimkia nchini Uturuki lakini mchakato wa usajili wake haukukamilishwa kwa wakati hivyo atalazimika kusubiri mwezi Januari
Imeelezwa kuwa Banda amesaini mkataba wa muda mfupi kuitumikia Nyasa Big Bullets wakati akisubiri dili lake la kutimkia Ulaya
Jana aliitumikia Nyasa Big Bullets katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Civil Service Utd akiisaidia timu yake mpya kupata ushindi wa mabao 3-2
