Licha ya klabu ya Chippa United kufungwa 3-2 dhidi ya Royal Am katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Afrika Kusini, kiungo Mtanzania Baraka Majogoro amegeuka kuwa lulu na kufikia kuimbwa kwenye mchezo huo baada ya kumalizika
Baada ya kujiunga na Chippa, Majogoro alikaa benchi kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Kaizer Chief uliomalizika kwa suluhu na baada ya hapo alikosekana kwenye mechi mbili mfululizo dhidi ya TS Galaxy 0-0 na Orlando Pirates 1-1.
Majogoro alirejea kikosini kwenye mchezo dhidi ya Mamelod Sundowns akikaa benchi na akishuhudia timu yake ikifungwa 2-0 lakini mechi ya tano dhidi ya Cape Towns Spurs alicheza dakika 90 na timu yake ikishinda 1-0.
Baada ya kiwango alichokionyesha kwenye mechi hiyo, Majogoro aliaminiwa katika mchezo wa Jumatano dhidi ya Royal AM akicheza dakika 90 huku timu yake ikipoteza 3-2.
Majogoro ni mchezaji wa pili Tanzania kucheza timu hiyo baada ya msimu uliopita kucheza Abdi Banda