Simba yaichapa Kipanga 3-0 mechi ya kirafiki

Joel JJ By Joel JJ β€’ 2nd September 2023


Simba yaichapa Kipanga 3-0 mechi ya kirafiki

Leo katika uwanja wa Mo Simba Arena ulioko Bunju nje ya kidogo ya jiji la Dar es salaam, klabu ya Simba ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kipanga Fc kutoka visiwani Zanzibar

Wekundu wa Msimbazi wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo huo uliopigwa asubuhi

Wafungaji wa mabao hayo ni Moses Phiri, Aubin Kramo na Luis Miquissone

Katika mchezo huo kipa mpya wa Simba Ayoub Lakred aliingia dakika ya 41 kuchukua nafasi ya Ally Salim

Ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Simba kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi dhidi ya Power Dynamos ya Zambia


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.