Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Septemba 05 2023

Joel JJ By Joel JJ
5 Sep 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Septemba 05 2023

Ujumbe wa Saudi Arabia uko nchini Uingereza kufanya jaribio la mwisho la kuishawishi Liverpool kumuuza Mohamed Salah kwa pauni milioni 200 kabla ya Alhamisi, huku kukiwa na imani kwamba mshambuliaji huyo wa Misri mwenye umri wa miaka 31 yuko tayari kujiunga na Al-Ittihad. (Mail)

Besiktas wanakaribia kukamilisha dili la winga wa Arsenal na Ivory Coast Nicolas Pepe, 28, kwa ada ya kawaida. (90 min)

Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 23, atajipata nje ya Manchester United msimu huu kama hatapata njia ya kutorokea Saudi Arabia, anasema beki wa zamani wa klabu hiyo Rio Ferdinand. (Telegraph - usajili unahitajika)

Mlinzi wa zamani wa Uhispani Sergio Ramos, 37, amekataa ofa ya mwisho ya kujiunga na Manchester United kabla ya kufikia mkataba wa kurejea Sevilla. (Sun)

West Ham wanatarajiwa kuwasilisha dau la kumsajili kwa muda mfupi kiungo wa England Jesse Lingard, 30, wakati wa mapumziko ya michuano ya kimataifa. (Mail)

Al-Ettifaq wanapania kumsajili winga wa Everton na Jamaica, Demarai Gray, 27, huku mchezaji huyo akitamani kuondoka Goodison Park. Nahodha wa Newcastle United Jamaal Lascelles, 29, ananyatiwa na klabu ya Al-Shabab inayoshiriki Ligi ya Saudia.(Team Talk)

Anderlecht wanakaribia kumsajili Kasper Schmeichel, 36, baada ya kuondoka Nice wiki jana. Kipa huyo wa Denmark alivutia Chelsea, Nottingham Forest na Brentford msimu wa joto. (Mail)

Manchester United bado wanajaribu kuwauza beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 29, na kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 26, huku kipindi cha usajiliwa wa wachezaji katila la Ligi ya Saudia kikielekea kufungwa siku ya Alhamisi. (Sun)

Kipa wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris, 36, anatazamiwa kusalia katika klabu hiyo hadi angalau Januari baada ya kukataa ofa nyingi msimu wa joto. (Standard)

BBC

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
1h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
3h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
3h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
5h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →